DRC-UNICEF-EBOLA-AFYA

Ebola: Mtu wa pili mwenye virusi vya Ebola apatikana Goma

DRC: Zoezi la chanjo kwa watoto dhidi ya Ebola katika kituo cha afya cha Himbi, Goma, 17 Julai 2019.
DRC: Zoezi la chanjo kwa watoto dhidi ya Ebola katika kituo cha afya cha Himbi, Goma, 17 Julai 2019. © REUTERS/Olivia Acland

Kesi ya pili ya maambukizi ya virusi vya Ebola imeripotiwa katika mji wa Goma, jiji kubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwenye mpaka na Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Katika mjji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, wenye wakaazi milioni 2, siku 16 zilizopita alipatikana mtu wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Ebola, ugonjwa ambao tayari umeua watu1,790 katika mkoa wa Ituri.

Kwa upande wake, shirika linalohudumia watoto (UNICEF) linasema lina wasiwasi na idadi ya watoto walioathiriwa na ugonjwa huo. Kati ya wagonjwa 2700 waliorodheshwa hadi leo, zaidi ya 25% ni watoto.

Kesi hii mpya ya maambukizi ya Ebola katika mji wa Goma, imegunduliwa. Inaripotiwa kuwa mgonjwa huyo wa Ebola ni mwanamume ambaye alikuwa akihudumiwa na wauguzi wa Bunia lakini akatoroka timu za wauguzi.