DRC-RWANDA-UGANDA-EBOLA-AFYA

Ugonjwa Ebola waendelea kuzua hofu kwa majirani wa DRC

Mpaka kati ya DRC na Rwanda ulifungwa kwa uamuzi wa serikali ya Kigali Alhamisi, 1 Agosti, 2019, wakati mji wa Goma unaendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola.
Mpaka kati ya DRC na Rwanda ulifungwa kwa uamuzi wa serikali ya Kigali Alhamisi, 1 Agosti, 2019, wakati mji wa Goma unaendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola. REUTERS/Djaffer Sabiti

Rwanda ilifunga mpaka wake na DRC kwa muda wa masaa kadhaa Alhamisi wiki hii, siku moja baada ya mgonjwa watatu aliyeambukizwa virusi vya Ebola kubainika katika mji wa Goma, ulio kwenye mpaka na Rwanda, mwashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Mpaka huo hata hivyo ulifunguliwa jioni kwa mujibu wa taarifa kutika Wizara ya afya.

Awali kulikuwa na wasiwasi kuwa mgonjwa aliyegudulika mjini Goma alikuwa amekutana na watu wengi na hivyo, kulikuwa na wasiwasi wa kusambaa kwa maambukizi hayo.

Aidha serikali ya Rwanda imekanusha uvumi ulioanza kuenea nchini humo kwamba, kuna kesi ya watu wawili waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Rubavu baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa Ebola

Uganda kwa upande wake, inasema hakuna maambulizi yoyote ya Ebola yaliyoripotiwa tena nchini humo, baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano aliyekuwa ameambukizwa kuvuka mpaka na kuingia nchini humo kabla ya kurudishwa tena makwao ndani ya mwaka mmoja wa maambukizi ya ugonjwa huu.

Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, yanaendelea kuongezeka, Mashariki mwa DRC, mwaka mmoja, baada ya kuzuka kwa ugonjwa huu hatari.

Watu zaidi ya 1,800 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2,000 kuambuakizwa virusi vya ugonjwa huo, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO), huku maambukizi mapya 15 yakitangazwa siku ya Jumatano.

Wakati huo huo Timu za kukingia ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Kivu Kusini zimetoa chanjo kwa watu arobaini waliotengwa kwa mara ya kwanza katika mkoa huo tangu kuibuka kwa Ebola mashariki mwa DRC.