DRC-EBOLA-AFYA

Maafisa wakuu wa afya DRC kuzuru eneo linalokumbwa na Ebola DRC

Vituo vya huduma ya dharura katika kituo cha matibabu cha Ebola cha shirika la matibabu la kibinadamu la Alima Beni, mashariki mwa DRC.
Vituo vya huduma ya dharura katika kituo cha matibabu cha Ebola cha shirika la matibabu la kibinadamu la Alima Beni, mashariki mwa DRC. REUTERS/Baz Ratner

Maafisa wakuu wa afya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo Jumatatu wanatarajia kutembelea mji wa Beni katika jimbo la Kivu kaskazini kutathmini hali ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa baada ya kamati maalum inayopambana na uginjwa huo kutangaza mikakati mipya ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa huu ambao umesababisha vifo zaidi ya watu 1,800 na wengine zaidi ya 2000 kuambukizwa mashariki wma DRC kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Dokta Jean Jacques Muyembe ni mkuu wa jopo-kazi linalopambana na Ebola katika serikali ya DRC anasema chanjo mpya ya Ebola imepatikana huku akiwaonya watu wanaoathiriwa na ugonjwa huu kujitokeza mara moja, bila ya kuchelewa.

Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, yanaendelea kuongezeka, Mashariki mwa DRC, mwaka mmoja, baada ya kuzuka kwa ugonjwa huu hatari.

Watu zaidi ya 1,800 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2,000 kuambuakizwa virusi vya ugonjwa huo, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO), huku maambukizi mapya 15 yakitangazwa siku ya Jumatano.