GABON-MAZINGIRA-USALAMA-AFYA

Maafisa usafi wa mji wa Libreville waendelea na mgomo, raia wapandwa na hasira

Mbele ya shule ya umma ya Nzeng Ayong katika wilaya ya 6 ya Libreville, taka zinasambaa barabarani, Agosti 7, 2019.
Mbele ya shule ya umma ya Nzeng Ayong katika wilaya ya 6 ya Libreville, taka zinasambaa barabarani, Agosti 7, 2019. RFI/Yves-Laurent Goma

Ndani ya siku kumi nchi ya Gabon itasherehekea siku yake ya uhuru. Kwa muda wa wiki moja, mji mkuu wa Gabon, Libreville, umeendelea kuwa na harufu mbaya na kuzungukwa, kila mahala, na marundo ya taka baada ya wahudumu wa kushughulikia usafi mjini Libreville kuanzisha mgomo.

Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Averda inayohusika na kusafisha mji wa Libreville inaendelea na mgomo ikidai malipo ya miezi 24 ya malimbikizo sawa na Faranga za FCFA bilioni 21.

Raia wamealamikia marundo ya taka, huku baadhi yao wakipandwa na hasira wakiomba serikali kuondoa taka hizo kwa hofu ya kutokea mlipuko wa magongwa mbalimbali, kama vile Kipindupindu na magonjwa mengine hatari yanayotokana na mazingira machafu.

Wafanyabiashara wengi wanasema wamepoteza wateja wengi kutokana na ukosefu wa usafi karibu na maeneo wakofanyia kazi.

"Ni ukweli usiopingika kuwa nchi ni chafu, hii ni kutokana na marundo ya taka ambayo yako katika mitaa mbalimbali hasa jijini Libreville na katika baadhi ya maeneo, na kuwa kero kutokana na harufu yake. Mrundikano huo ni kutokana na mgomo wa wahudumu wa kufanya usafi wa mji, " amesema Sonia mmoja wa wafanyabiashara hao.

"Kampuni ya usafi ya Averda inayohusika na kusafisha mji wa Libreville imeamua kutia mgomo baridi wa kubeba taka hizo na kuzipeleka katika madampo husika, " ameongeza Sonia.

Kampuni ya Averda inayohusika na usafi wa mji inanajua madhara ya taka hizo kwa wananchi lakini inaweka shinikizo ili iweze kulipwa.

Nicolas Achkar, mkurugenzi wa maendeleo wa Averda amesema. "Leo tunahitaji mpango wa kulipwa deni na malipo yawe haraka ili turudi kazini,"

Kwa upande wake Serge William Akassaga, naibu wa kwanza wa meya wa Libreville anasema amesikitishwa na uamuzi huo wa kampuni ya Averda wa kusitisha kazi.

"Gabon ni nchi huru ambayo hatutokubali shinikizo lolote kutoka kwa kampuni na mbinu mbovu za Averda! ".

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, wahudumu wa kufanya usafi wa kampuni ya Averda walifanya tena mgomo kama huo wakidai malipo ya malimbikizo.