MAREKANI-TABIA NCHI-MAZINGIRA

Marekani yarasimisha mchakato wa kujitoa kwenye mkataba wa Paris

Donald Trump alitangaza azma yake ya kujiondoa kwenye mkataba huo, ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa hewa chafu.
Donald Trump alitangaza azma yake ya kujiondoa kwenye mkataba huo, ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa hewa chafu. REUTERS/Joshua Roberts

Serikali ya Marekani imewasilisha barua yake kwenye Umoja wa Mataifa na kusahihisha rasmi uamuzi wake wa kujtoa kwenye mkataba wa tabia nchi, ikithibitisha ahadi yake.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imeanza rasmi mchakato wa kujitoa kwenye mkataba wa Paris kuhusu tabianchi. Barua hiyo ilikuwa ikisubiriwa tangu mwaka 2017, lakini haingeweza kutumwa mapema, kwani hakuna nchi ambayo ingeweza kujitoa kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kuanza kutumika mkataba huo Novemba 4, 2016.

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa mpinzani mkubwa wa makubaliano hayo wakati alipokuwa anawania kiti cha urais, na utawala wake umekuwa ukifanya kila unaloliweza kubadilisha sheria za mazingira, ukisema zinazuwia biashara na kutoa kwa nchi nyingine nguvu ya ushindani.

Karibu mataifa 200 yalisaini mkataba huo wa mazingira ambapo kila nchi inatoa malengo yake ya kupunguza utoaji wa hewa chafu inayosababisha na mabadiliko ya tabianchi.

Donald Trump ametangaza nia yake ya kujitoa kwenye mkataba huo, ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

"Leo, Marekani inaanza mchakato wa kujiotoa kwenye mkataba wa Paris. Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo, Marekani imesahihisha rasmi kwenye Umoja wa Mataifa uamuzi wake wa kujitoa kwenye mkataba huo. Mchakato huo utakamilika mwaka mmoja baada ya ya uamuzi huo kusahihishwa, " Waziri wa Mambo ya Njee wa Marekani Mike Pompeo amesema katika taarifa.

Taarifa ya Pompeo ilielezea kuhusu kile alichokiita "mzigo usio wa haki wa kiuchumi uliowekwa kwa wafanyakazi wa Marekani, biashara, na walipa kodi, kwa ahadi za Marekani zilizotolewa chini ya makubaliano hayo".