RWANDA-EBOLA-AFYA

Zoezi la kutoa chanzo dhidi ya Virusi vya Ebola laendelea Magharibi mwa Rwanda

Mwanamke huyu akiosha mikono yake katika eneo la ukaguzi wa Ebola kabla ya kuingia DRC akitokea Rwanda huko Goma, Julai 16, 2019.
Mwanamke huyu akiosha mikono yake katika eneo la ukaguzi wa Ebola kabla ya kuingia DRC akitokea Rwanda huko Goma, Julai 16, 2019. JOHN WESSELS / AFP

Wakati nchi ya Rwanda ikiendelea kutoa chanjo ya Ebola katika mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika Wilaya ya Rubavu, wengi wanahofia chanjo hiyo licha ya wito unaoendelea kutolewa na maafisa wa afya.

Matangazo ya kibiashara

Katika kituo cha kutolea chanjo kilichotengwa mpakani, ambako mwandishi wetu Edith Nibakwe, ametembelea wananchi wameendelea kupewa maelezo kuhusu chanjo hiyo ya Ebola na wale wanaokubali wamepewa chanjo ya kwanza ya ugonjwa huo.

“Wananchi wanaendelea kuitikia wito uliyotolewa na maafisa wa afya” amesema Daktari Kanyankore Williams, Mkurugenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Gisenyi, ambaye pia hufuatilia zoezi hilo.

“Tumefanikiwa pia kuzungumza na badhii ya wananchi ili kujua wanapokeaje zoezi hilo ,baadhi yao wameonyesha hofu ya kupewa chanjo kutokana na maneno yanayozungumzwa mitaani” , ameongeza Daktari Kanyankore.

Aidhaa Dkt Kanyankore Williams, amewatoa hufu wanachi ambao wanaendelea kusikia maneno hayo na kusema zoezi hilo ni njia moja ya kuwalinda Wanyarwanda dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola

Tangu kuanza kwa zoezi hilo watu zaidi elfu nane ndio waliojitokeza kupewa chanjo hiyo ya kwanza. Raia  wasiopungua 200,000  ndio wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo katika wilaya za Rubavu na Rusizi. 

Wafanyakazi wa afya ,maafisa wa uhamiaji, polisi na raia hasa wanaojihusisha na biashara ya mipakani ndo wanapewa nafasi ya mbele kupata chanjo hiyo.

Chanjo hutolewa kwa hiari ya kila mtu na mashrti yaliyopo ni kwamba chanjo inapewa mtu ambaye yuko tayari kupewa chanjo ya pili kwani ni sharti mtu apewe kinga mara mbili, kwa mujibu wa chanzo cha afya kutoka wilayani Rubavu.