Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vyaongezeka China

Mmoja wa wafanyakaziwa mji wa Wuhan, akifanyiwa vipimo vya joto katika hali ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona, Februari 1, 2020.
Mmoja wa wafanyakaziwa mji wa Wuhan, akifanyiwa vipimo vya joto katika hali ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona, Februari 1, 2020. China Daily via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

China imetangaza leo Alhamisi visa 15,000 vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa unaofahamika kama Corona, hali inayoendelea kuzua wasiwasi mkubwa nchini humo na ulimwenguni.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo maafisa wakuu wa Mkoa wa Hubei, ambako ugonjwa wa Corona ulianzia, wamefutwa kazi.

Takwimu hizi zinazotia wasiwasi na vikwazo hivi vya nidhamu vinachochea uvumi kwamba ukali wa ugonjwa huo wa matatizo ya kupumua unaosababishwa na virusi vya Corona, ambao kwa sasa unajulikana kama Covid-19, umekithiri.

Tume ya Afya katika Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, imetangaza vifo vipya vya watu 242 katika mkoa huo. Hii ni ongezeko kubwa zaidi llinaloshuhudiwa ndani ya saa 24 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mwezi Desemba katika mji mkuu wa mkoa huo wa Wuhan.

Mapema wiki hii shirika la Afya Duniani, WHO, lilitangaza ugonjwa wa Corona kama ni janga la dharura nchini China , lakini likaamua kutotangaza hali hiyo ya kiafya kama ilivyofanywa na ugonjwa wa homa ya nguruwe na Ebola.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.