Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

China yaendelea kukumbwa na ugonjwa wa Covid-19

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa unaofahamika kama Corona (Covid-19) inaendelea kuongozeka China na nje ya nchi hiyo.
Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa unaofahamika kama Corona (Covid-19) inaendelea kuongozeka China na nje ya nchi hiyo. China Daily via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mlipuko wa ugonjwa wa Corona unaofahamika sasa kama Covid-19 hauonyeshi dalili zozote za kupungua nchini China wakati maafisa wa afya nchini humo wamesema leo Ijumaa kuwa wameorodhesha zaidi ya kesi 5,000 za maambukizi mapya.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imekuja saa chache baada ya Washington kukosoa hatua za Beijing kuhusu kukabiliana na ugonjwa huo na kushtumu kwamba hakuna uwazi katika jitihada hizo.

Tume ya kitaifa ya Afya nchini China imetangaza leo Ijumaa kwamba imeorodhesha vifo vipya 121 na kupelekea idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Covid-19 kufikia zaidi ya 1, 423 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mwezi Desemba mwaka jana.

Katika taarifa yake, Tume ya kitaifa ya Afya nchini China imetangaza kwamba kesi 5,090 mpya za maambukizi ziliorodheshwa jana Alhamisi China Bara, ambapo idadi ya watu walioambukizwa sasa imefikia 65,851 kulingana na takwimu zake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.