Pata taarifa kuu
NIGERIA-CORONA-AFYA

Kesi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 yathibitishwa Nigeria

Raia mmoja wa Italia aliyerudi kutoka Milan Februari 25 alilazwa hospitalini baada ya kupimwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 katika Jimbo la Lagos.
Raia mmoja wa Italia aliyerudi kutoka Milan Februari 25 alilazwa hospitalini baada ya kupimwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 katika Jimbo la Lagos. Photo: Jane Barlow/Pool/AFP

Raia wa Italia ambaye aliwasili nchini Nigeria siku tatu zilizopita amepatikana na virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini humo. Taarifa hiyo imetolewa na Wizara ya Afya ya Nigeria, wakati janga hilo linaendelea kusambaa haraka kote duniani.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi hivyo kutbitishwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Raia huyo wa Italia ambaye aliwasili nchini Nigeria akitokea Milan Februari 25 alilazwa hospitalini baada ya kupimwa virusi vya ugonjwa Covid katika Jimbo la Lagos, ambapo mji mkuu wa jimbo hilo una wakazi milioni 20.

Ni mgonjwa wa kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara, Wizara ya Afya ya Nigeria imesema katika taarifa yake leo Ijumaa: "Mgonjwa yuko katika hali nzuri na hana dalili za kutatanisha. "

Italia inaendelea kuonekana kama eneo la usambazaji wa virusi vya Covid-19. Mataifa mengi ya Ulaya yameimarisha hatua zao za kuzuia maambukizi ya virusi hivyo na kuwashauri raia wao wasiende katika mikoa iliyoathirika ya Italia. Roma imechukua hatua kali, ikiwa ni pamoja na hatua ya kuweka karantini wilaya 11 za Kaskazini.

Kwa upande mwingine, Nigeria ni nchi ambayo ina uhusiano tosha na China, kwani Wanigeria wengi husafiri kwenda kufanya biashara. Hii ndio sababu viongozi wa Nigeria walichukuatahadhari mapema. Mamlaka nchini Nigeria imebaini kwamba vituo vya kuwapokea watu walio na dadili za ugonjwa huo vimejengwa katika miji ya Lagos na Abuja.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.