CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuwa kitisho duniani

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa hatari unaofahamika kama Covid-19 duniani imezidi watu 3000, baada ya mamlaka nchini China kutangaza Jumatatu asubuhi Machi 2 vifo vipya vya watu 42 katika jimbo la Hubei, katikati mwa China, ambapo ugonjwa huo ulianzia.

Kesi mpya 500 za maambukizi zimeripotiwa nchini Italia kati ya Februari 29 na Machi 1.
Kesi mpya 500 za maambukizi zimeripotiwa nchini Italia kati ya Februari 29 na Machi 1. REUTERS/Yara Nardi
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa afya wa China wametangaza leo Jumatatu kuwa wamethibitisha kesi mpya 202 za maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 katika China Bara, na kutimiza watu 80,026 walioambukizwa virusi hivyo tangu ugonjwa huo ulianza mwezi Desemba 2019.

Mlipuko wa ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 2,912 nchini china tangu kuzuka kwake, kulingana na takwimu za serikali.

Ugonjwa huo hatari unaendelea kusambaa katika bara la Ulaya.

Baada ya Ireland, Luxembourg na Armenia, Jamhuri ya Czech ilitangaza jana Jumapili mtu wa kwanza kupatikana na virusi vya Covid-19 nchini humo. Ni mtu watatu ambaye alitembelea Kaskazini mwa Italia aliyepatikana na virusi hivyo. Jamhuri ya Dominika imekuwa nchi ya nne katikaukanda wa Amerika ya Kusini kuathiriwa na ugonjwa huo.