JAPAN-CORONA-AFYA

Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuiathiri Japan

Mamlaka ya Japani inajitahidi kukabiliana na virusi hivyo wakati nchi hiyo inajianda kupokea michuano ya kimataifa ya Olimpiki msimu huu wa joto. Zaidi ya kesi 40 zimeripotiwa katika mji mkuu wa Japan, Tokyo.
Mamlaka ya Japani inajitahidi kukabiliana na virusi hivyo wakati nchi hiyo inajianda kupokea michuano ya kimataifa ya Olimpiki msimu huu wa joto. Zaidi ya kesi 40 zimeripotiwa katika mji mkuu wa Japan, Tokyo. REUTERS

Kesi za maambukizi ya virusi vya Covid-19 zilizothibitishwa nchini Japan zimefikia kiwango cha juu cha watu 1,000 baada ya kesi mpya kuripotiwa katika mkoa wa Yamaguchi magharibi mwa nchi, wawakilishi na waandishi wa habari wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Virusi hivyo vimeuwa watu 12, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya.

Mgonjwa wa mwisho aliyepatikana na virusi vya ugonjwa huo ni mtu mwenye umri wa miaka arobaini, Gavana wa Mkoa wa Yamaguchi, Tsugumasa Muraoka, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Hii ni kesi ya kwanza kuthibitishwa katika mkoa huu, na kuonyesha jinsi gani ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuenea nchini kote.

Mamlaka ya Japani inajitahidi kukabiliana na virusi hivyo wakati nchi hiyo inajianda kupokea michuano ya kimataifa ya Olimpiki msimu huu wa joto. Zaidi ya kesi 40 zimeripotiwa katika mji mkuu wa Japan, Tokyo.

Kati ya watu elfu moja walioambukizwa virus vya ugojnwa wa Covid-19 nchini Japan tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, 706 walikuwa katika meli ya abiria ya Princess Princess, iliyozuia katika bandari ya Yokohama, karibu na mji mkuu wa Tokyo, mapema mwezi Februari mwaka huu.