SENEGAL-CORONA-AFYA

Kesi mbili mpya za maambukizi ya virusi vya Covid-19 zathibitishwa Senegal

Senegal nchi ya nne barani Afrika ambayo inaendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugojnwa wa Covid-19 imetangaza kesi mbili mpya za maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo nchini humo.

Wagonjwa wawili wapya wa Coronawamewekwa karantini katika Hospitali ya Fann, Dakari, Senegal.
Wagonjwa wawili wapya wa Coronawamewekwa karantini katika Hospitali ya Fann, Dakari, Senegal. Seyllou / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesi mbili mpya za maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 zimegunduliwa Jumatano, Machi 4. Miongoni mwa watu hao walioambikizwa virusi hivyo ni pamoja na mwanamke wa mmoja wa wagonjwa wanaoendelea kuhudumiwa, ambaye anaishi nchini Ufaransa. Mgonjwa mwingine ni raia wa Uingereza, ambaye alitoka London wiki moja iliyopita. Wote wawili wamewekwa karantini katika Hospitali ya Fann.

Mgonjwa wa pili aliyepatikana na virusi vya Corona aliamuambukiza mkewe katika kitongoji cha Dakar cha Guédiawaye, kwa mujibu wa vyanzo kutoka hospitali.

Jumatano hii, vipimo vilivyofanywa na taasisi moja nchini Senegal, Institut Pasteur, vinaonyesha kuwa mwanamke wa miaka 68 pamoja na mumewe wa miaka 80, ambao walikuwa wamekuja kuhudhuria mazishi ya mpendwa wao huko Guédiawaye wamepatikana na virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Uchunguzi ulifanyika papo hapo ili kujaribu kupata watu waliokuwa nao karibu.

Serikali ya Senegal imewataka raia kutoa ushiriki wao kwa kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo unaotia wasiwasi dunia.