Marekani yatoa dola bilioni 8.3 kwa kukabiliana na Virusi vya Covid-19
Imechapishwa:
Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha mpango wa dharura wa dola bilioni 8.3 ili kufadhili vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kusambaa nchini Marekani na mataifa mengine duniani.
Bunge la Seneti limepitisha kwa kauli moja mpango huo wa dharura, wakati Marekani ikiendelea kupambana dhidi ya kuendea kwa virusi vya ugonjwa hatari vay Covid-19.
Rais Donald Trump alikuwa amependekeza bajeti ya kwanza ya dola bilioni 2,5, iliyochukuliwa na chama cha upinzani cha Democratic kuwa haitoshi kwa kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo.
Mpango huo unakusudia kuboresha hatua ya mamlaka na kufadhili hasa utafiti na maendeleo ya chanjo, matibabu, na huduma za matibabu za mbali.