RWANDA-CORONA-AFYA

Rwanda yachukua hatua za kukabiliana na virusi vya Corona

Rwanda imeanzisha mikakati kabambe ya kupambana na ugonjwa wa Corona. Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kanombe uliopo jijini Kigali, umezungukwa na kamera za kisasa (CCTV).

Uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali, Rwanda
Uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali, Rwanda en.wikipedia.org
Matangazo ya kibiashara

Kamera hizo zilizounganishwa na kompyuta zina uwezo wa kupima virusi ya Corona kwa kila mtu anayeingia pasipo kumgusa na kujua kama ana maambukizi au la.

Kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa kanombe jijini Kigali, watu wanaingia na kutoka bila hofu yoyote ya kuambukizwa virusi vya Covid-19.

Kadri wanavyoingia kwenye uwanja huo wa ndege, ndivyo kamera zilizowekwa uwanjani hapo zinafanya kazi ya kupima joto ya kila mtu anayeingia pasipo kuguswa na kutoa taarifa ya joto lake kwenye kompyuta zilizounganishwa na kamera hizo.

Mtu anayepatiakana na virusi vya ugonjwa wa Corona anachukuliwa na karantini.

Kwa wale wanaoingia bila kupimwa joto, wanapaswa kufika mbele ya madaktari, kila mtu wakimhoji ili kujua kama nchi alikotoka imewahi kuripoti kesi za ugonjwa wa Covid-19 au la.

Watu walioingia kutoka nje ya taifa hilo, wanasema wamefurahishwa na zoezi la kupima joto pasipo kusogelewa na mtu.

“Nimefurahishwa zoezi hilo na nalioaona hapa Kigali na ninahisi hii ni njia bora ya kupima joto, laiti upimaji wa namna hiyi ungeenea duniani kote idadi ya maambkizi ya Corona ingepungua” , mmoja wa raia wa kigeni aliyepata huduma hiyo amebaini.

Mamlaka nchini Rwanda inasema kamera hizo zimerahisisha sana zoezi la kupima joto kwa watu wanaoingia nchini humo kutoka mataifa ya nje.

“Unapowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe kamera zinahisi kama kuna mtu ambaye amingia kwenye eneo hilo na kumtaka kufanya vipimo vya joto bila kusogeleana na mtu yeyote.

Mufumo huu umerahisisha kwa kiasi kikubwa zoezi hili kupima watu wanoingia chini” , amesema Dkt Jose Nyamusore

Hadi sasa Rwanda haijaripoti kisa chochote cha virusi vya ugonjwa wa Covid-19, japokuwa zaidi ya watu elfu themanini wameripotiwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo katika nchi 40 duniani.

Ripoti ya Bonaventure Cyubahiro