UGANDA-AFYA-CORONA

Coronavirus: Uganda kuwarudisha raia wa kigeni 22 katika nchi zao

Baadhi ya nchi za bara la Afrika zimezidisha hatua za kiafya kwa ajili ya kukabiliana na maambukizo ya virusi hatarishi vya corona, huku jitihada zikiendelea ndani ya nje ya China kwa ajili ya kutafuta tiba ya ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo.
Baadhi ya nchi za bara la Afrika zimezidisha hatua za kiafya kwa ajili ya kukabiliana na maambukizo ya virusi hatarishi vya corona, huku jitihada zikiendelea ndani ya nje ya China kwa ajili ya kutafuta tiba ya ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo. REUTERS/Edward Echwalu

Wizara ya afya nchini Uganda imesema raia wa kigeni 22 waliokuwa wamewasili nchini humo kutoka katika mataifa yaliyoathiriwa na maambukizi ya Corona na kuombwa kutengwa kwa siku 14 watarudishwa katika nchi zao baada ya kukataa utaratibu huo wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Wageni hao walikuwa wamewasili nchini humo kuhudhuria mkutano wa kibiashara kati ya Uganda na bara Ulaya ambao unaanza leo na kumalizika kesho.

Waziri wa Afya wa Uganda Ruth Aceng, pia ametangaza mataifa ambayo raia wake hawataruhusiwa nchini humo kwa sasa.

Mapema mwezi Februari wasafiri zaidi ya 100 waliwekwa karantini baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala nchini Uganda wakitokea nchini China.

Raia 44 wa China ni miongoni mwa wasafiri hao waliotengwa.

Wakati huo mamlaka ya uwanja wa ndege nchini nchini humo ilisema uamuzi huo ulichukuliwa ili kuepusha hatari ya maambukizo ya virusi vya corona ambavyo husababisha maafa muda mfupi baada ya mtu kuambukizwa.

Naye Waziri wa Afya wa Uganda, Dakta Jane Aceng alisema watu zaidi ya 100 kutoka nchini China wamewekwa kwenye karantini na watasalia katika hali hiyo ya kutengwa kwa muda wa siku 14 ili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya katika hospitali na vituo mbalimbali vya kiafya nchini humo. Dakta Aceng ameongeza kuwa, miongoni mwa wasafiri hao waliotengwa ni raia 44 wa China.

Virusi hatari vya corona vilianza kujitokeza kwa mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka jana 2019 katika mji wa Wuhan, mkoani Hubei nchini China na kuenea katika maeneo mengine ya dunia.