ITALIA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 yaongezeka Italia

China bara ambako ndiyo chimbuko la virusi vya Corona  pamoja na Korea Kusini, Iran na Italia ndiyo mataifa yenye visa vingi vya maambukizi lakini maambukizi yameshuhudiwa pia katika mataifa mengine zaidi ya 40 duniani.
China bara ambako ndiyo chimbuko la virusi vya Corona pamoja na Korea Kusini, Iran na Italia ndiyo mataifa yenye visa vingi vya maambukizi lakini maambukizi yameshuhudiwa pia katika mataifa mengine zaidi ya 40 duniani. Marzio Toniolo / via REUTERS

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana maambukizi ya Corona nchini Italia, imeongezeka na kufikia watu 197 wakati huu serikali ikijaribu kuwatenga watu Milioni 16 katika eneo la Lombardy na mikoa 14.

Matangazo ya kibiashara

Mripuko wa virusi vya Corona nchini Italia ndiyo mbaya zaidi barani Ulaya na kwa sehemu kubwa umeyakumba maeneo ya Kaskizini ya taifa hilo.

Hivi sasa bara la Ulaya linashuhudia kuongezeka maambukizi baada ya Serbia na Vatican kurekodi visa vya kwanza vya Corona.

Idadi ya wagonjwa walio mahututi imefikia watu 426 na ongezeko hilo limeleta wasiwasi wa kukosekana vitanda zaidi vya kuwalaza wagonjwa wanaohitaji  msaada wa dharura, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Deutsche Welle (DW).

Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha  Johns Hopkins University nchini Marekani pamoja na tarakimu kutoka vyanzo vingine zinasema idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imepindukia watu 100,000 kote duniani.

Maambukizi zaidi yameripotiwa pia nchini Uingereza, Ufaransa, Uswisi, Ujerumani pamoja na Croatia.

Mjini Geneva, Shirika la Afya Duniani WHO limesema takwimu zake zinaonesha mamabukizi yamefikia watu 98,023 huku Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo akisema ulimwengu " uko kwenye ukingo wa kufikia maambukizi 100,000."