RWANDA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Mikusanyiko ya watu wengi yapigwa marufuku Kigali

Moja ya mitaa ya katikati mwa mji wa Kigali.
Moja ya mitaa ya katikati mwa mji wa Kigali. RFI/Laure Broulard

Utawala wa serikali za mitaa jijini Kigali nchini Rwanda umepiga maarufuku mikutano ya watu wengi jijini kama hatua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corana,japo Rwanda haijathibitisha kisa chochote cha maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari utawala wa jiji hilo ilisema mikutano kala vile tamasha ya muziki,maonyesho ya kibiashara au mikutano yenye umati kubwa imesitishwa kwa muda.

Hayo yanajiri wakati Tunisia imethibitisha visa vingine vitatu vya maambukizi ya virusi vya Corona na kuongeza idadi kamili ya watu waliomabukizwa kufikia watano.

Maafisa wa afya nchini humo wamesema visa hivyo vya hivi punde vimeripotiwa katika mji wa Bizerte na wawili wa wagonjwa hao wanasemekana walikuwa wemesafiri kwenda Italia.

Na kwingineko barani Afrika, nchini Afrika Kusini watu saba wamebainika kuambukizwa virus vya Corona baada ya kurejea kutoka nchini Italia walikoenda kufanya Utalii.

Akizungumzia visa hivyo vya maambukizi mapya katika Jumuiya ya Maendeleo ya

nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Idara ya Afya ya Afrika kusini Dakta Patrick Moonasar, amesema wameanza kuchukua hatua.

Kufikia sasa nchi nane barani Afrika zimethibitisha uwepo wa virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19.