MONGOLIA-CORONA-AFYA

Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Covid-19 chathibitishwa Mongolia

Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona charipotiwa Mongolia.
Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona charipotiwa Mongolia. © Site de l’UNCCD

Raia wa Ufaransa anayefanya kazi nchini Mongolia amepatikana na virusi vya ugonjwa wa Covid-19, viongozi wa afya wa eneo hilo wameripoti leo Jumanne, wakisema ni kisa cha kwanza kuthibitishwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya kitaifa ya uokoaji imesema mgonjwa, raia wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 57, aliwasili nchini humo kutoka Ufaransa baada ya kupitia Moscow, anaendelea vizuri.

Serikali imebaini watu 42 ambao mgonjwa alikutana nao na watu wengine 120 aliowasiliana nao kwa karibu, tume hiyo imesema katika taarifa.

Shughuli za aina yoyote katika mkoa wa Dornogovi, ambapo mgonjwa huo anaendelea kuhudumiwa, zimesitishwa, tume hiyo imeongza.

Katika kujaribu kuzuia kuenea kwa janga hilo, mamlaka nchini Kimongolia ilikuwa imeweka hatua za ukaguzi kwenye mipaka yake na kuzuia wasafiri wanaotoka au kuingia China.

Mipuko wa ugonjwa wa Covid-19 ulianzia China na kuenea duniani.

Chini ya mwezi mmoja, virusi vya Corona viliripuka kuwa janga kubwa la afya na kuwaua watu karibu 500 na kuwaathiri karibu wengine 6,000. Wanasayansi wanahangaika kutafuta chanjo ya kukabiliana nacho.

Desemba 31, 2019 China ililiarifu Shirika la Afya Duniani, WHO, kuhusu visa vya maambukizi ya virusi kwenye mji wa Wuhan ulio na wakaazi milioni 11. Mzizi wa virusi hivyo haukujulikana na wataalamu wa maradhi duniani kote wakaanza kufanya kazi ili kuvibaini. Chanzo kikabainika kuwa ni soko la vyakula vya baharini katika mji huo, na kufungwa kwa haraka. Watu 40 wakaripotiwa kuambukizwa.

Hata hivyo ugonjwa huo sasa unaendelea kuenea duniani kote, huku viongozi na raia wakiingiliwa na wasiwasi kutokana na hali hiyo.