DRC-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Covid-19 chathibitishwa DRC

Barabara inayotumliwa na watu wengi jijini Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu).
Barabara inayotumliwa na watu wengi jijini Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu). Photo by Ute Grabowsky/Photothek via Getty Images

Idadi ya kesi za maambukizi ya ya virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 inaendelea kuongezeka barani Afrika. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo unaendelea kutia wasiwasi viongozi mbalimbali duniani.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya wa DRC, Dkt Eteni Longondo amethibitisha taarifa hiyo, akibaini kamba mgonjwa, mwenye umri wa miaka 52, ambaye ni raia wa DRC "anaendelea vizuri".

Hata hivyo mgojnwa huyo amewekwa karantini, na anaendelea kupata huduma inayofaa katika kituo cha afya, kwa mujibu wa maafisa wa DRC, amesema waziri wa Afya Dkt Longondo, ambaye pia amebaini kwamba maafisa wa afya "watatafuta na kubaini wale wote ambao waliwasiliana na mgonjwa".

Raia huyo wa DRC aliyepatikana na virusi vya ugonjwa wa Covid-19 anaishi nchini Ufaransa. Kwa hivyo Mbelgiji, tofauti na iliyotangazwa awali.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Dk Eteni Longondo, alifika jijini Kinshasa Machi 8 akitokea nchini Ufaransa, ambapo anaishi.

Dkt Eteni Longondo ameongeza kuwa serikali na washirika wake wanafanya kila linalowezekana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Kwa hivyo, ametoa wito kwa raia kushirikiana na maafisa wa afya na timu za kukabiliana na magonjwa yanayoambukia.