UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Waziri wa afya nchini Uingereza Nadine Dorries akutwa na maambukizi

Mawaziri wote wa afya, akiwemo Waziri Mkuu wa afya Matt Hancock, watafanya vipimo, sambamba na maafisa wengine ambao walikaribiana na bi Dorries.
Mawaziri wote wa afya, akiwemo Waziri Mkuu wa afya Matt Hancock, watafanya vipimo, sambamba na maafisa wengine ambao walikaribiana na bi Dorries. UK Parliament/Jessica Taylor

Waziri wa Afya wa Uingereza na mbunge wa chama cha Conservative, Nadine Dorries, ametangaza katika taarifa kwamba ameambukizwa virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

"Ninaweza kuthibitisha kuwa nimekutwa na virusi vya ugonjwa wa Covid-19 (...) na kwamba nimejiweka peke yangu karantini nyumbani kwangu," amebaini waziri huyo mwenye umri wa miaka 62.

Bi Dorries, mbunge wa Bedfordshire ya kati, amesema katika taarifa yake kuwa Idara ya afya imeanza kuwafuatilia watu waliokuwa karibu naye, na ofisi yake ya bunge inafuatilia hilo kwa karibu.

Idara ya afya imesema alianza kuonesha dalili siku ya Alhamisi juma lililopita, alipohudhuria dhifa iliyofanyika Downing Street iliyohodhiwa na Waziri Mkuu Boris Johnson, na akawekwa karantini tangu siku ya Ijumaa.

Mawaziri wote wa afya, akiwemo Waziri Mkuu wa afya Matt Hancock, watafanya vipimo, sambamba na maafisa wengine ambao walikaribiana na bi Dorries, kwa mujibu wa chanzo kutoka serikali ya Boris Johnson.

Hali hii imekuja wakati kukiwa na taarifa ya kifo cha mtu wa sita aliyeambukizwa virusi vya Covid-19 nchini Uingereza ambako kunaripotiwa visa vya watu 382 waliombukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari.