Coronavirus Ufaransa: Shule zafungwa, uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika
Imechapishwa:
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza hatua mpya za kukabiliana za kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao Shirika la Afya Duniani lilitangaza kwamba ni janga la kimataifa.
Akihutubia taifa kwenye televisheni, rais Emmanuel Macron amewahakikishia wananchi wa Ufaransa kwamba hatua kadhaa zimechukuliwa ili kukabiliana na kuenea kwa janga hilo na "kulinda" watu ni rahisi kupata maambukizi ya virusi hivyo.
Moja ya hatua hizo na ambayo ni muhimu ni kufungwa kwa shule zote kuanzia zile za chekechea na vyuo vikuu, hatua ambayo itaanza kutekelezwa Jumatatu, Machi 16.
Rais wa Ufaransa pia amewataka "watu wote walio na umri wa zaidi ya miaka 70, wale wanaougua magonjwa sugu, walemavu, wabaki nyumbani. "
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, rais Macron ametangaza kwamba "hakuna kitu kinachomzuia Mfaransa yeyote, hata yule aliye hatarini zaidi, kwenda kupiga kura". duru ya kwanza ya uchaguzi huo itafanyika Jumapili hii Machi 15. Uamuzi uliochukuliwa, amesema Emmanuel Macron, kufuatia mkutano na wataalamu kadhaa katika ikulu ya Elysée.
Avant de s'adresser aux Français à 20h, le Président a réuni le Conseil scientifique mobilisé pour faire face au Coronavirus. Notre réaction ne peut se faire qu’avec l'expertise des spécialistes qui sont les plus légitimes pour évaluer la situation. pic.twitter.com/hoyvKclkbi
Élysée (@Elysee) March 12, 2020
Rais Emmanuel Macron amesema , janga hili "ambalo linaathiri mabara yote na nchi zote za Ulaya" ni "mgogoro mkubwa wa kiafya ambao Ufaransa haijawahi kushuhudia kwa kipindi chote cha karne moja".
Pia rais wa Ufaransa amesema yuko na kubaliana na hoja ya kufungwa kwa mipaka, lakini uamuzi huo utaamuliwa na "viongozi wa Ulaya".