CANADA-CORONA-AFYA

Mke wa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau apatikana na virusi vya ugonjwa wa Covid-19

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na mkewe Sophie Grégoire kabla ya sherehe ya kutawazwa kwa Waziri mkuu mpya, Novemba 4, 2015.
Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na mkewe Sophie Grégoire kabla ya sherehe ya kutawazwa kwa Waziri mkuu mpya, Novemba 4, 2015. REUTERS/Chris Wattie

Sophie Grégoire Trudeau, mkewe Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amepatikana na virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Matangazo ya kibiashara

Sophie Grégoire Trudeau ataendelea kusalia karantini "kwa muda usiojulikana," ofisi ya Waziri Mkuu Justin Trudeau imesema katika taarifa Alhamisi jioni wiki hii.

"Waziri Mkuu yuko katika afya njema na hana dalili zozote za maambukizi. Hata hivyo, kwa tahadhari na kulingana na ushauri wa madaktari, atawekwa karantini kwa muda wa siku 14, "kimebaini chanzo hicho, na kuongeza kuwa mkewe anaendelea" vizuri".

Justin Trudeau, 48, "kwa hivi sasa" hatafanyiwa vipimo na "ataendelea na majukumu yake kama Waziri Mkuu," ilisema ofisi yake, na kuongeza kuwa Waziri Mkuu atalihutubia taifa leo Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Canada aliwapigia simuwenzake wa Italia, Marekani na Uingereza Alhamisi mchana, ofisi yake imesema. Siku ya Ijumaa, atakutana na wasaidizi wake kutoka mikoa yote ya Canada ili kujadili jinsi gani ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, ambao umeshika kasi nchini Canada katika siku za hivi karibuni.

Zaidi ya kesi 150 ziliripotiwa nchini Canada Alhamisi wiki hii, hasa katika Jimbo la Ontario, katikati mwa nchi, na katika eneo la Magharibi, ambapo mtu mmoja alifariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Katika ujumbe kwa raia wa Canada, mkewe Justin Trudeau amewahakikishi raia kuwa anaendelea vizuri. Ofisi ya Waziri Mkuu imetangaza mapema asubuhi kwamba alifanyiwa vipimo vya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 kwa sababu alikuwa na dalili za Homa tangu kurudi kutoka London.

"Ingawa ninakabiliwa na dalili mbaya za virusi vya ugonjwa wa Covid-19, nina imani kwamba nitarudi katika hali yangu ya kawaida muda mfupi," amesema Sophie Grégoire Trudeau.