KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Serikali ya Kenya yapiga marufuku raia kutoka mataifa yaliyoathiriwa kuingia Kenya

Maafisa wa afya wa Kenya wakiwa wamevalia mavazi maalumu uyakujizuia maambukizi ya ugojnwa hatari wa Covid-19 yanayosababishwa na virusi vya Corona, katika mji wa Rongai karibu na Nairobi, Kenya Machi 14, 2020.
Maafisa wa afya wa Kenya wakiwa wamevalia mavazi maalumu uyakujizuia maambukizi ya ugojnwa hatari wa Covid-19 yanayosababishwa na virusi vya Corona, katika mji wa Rongai karibu na Nairobi, Kenya Machi 14, 2020. REUTERS/Baz Ratner

Serikali ya Kenya imetangaza mikakati mipya ya kupambana na maambukizi ya Corona, baada ya idadi ya watu walioambukizwa kufikia watatu jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta ni pamoja na kuzuia wageni kuja nchini humo kutoka mataifa yaliyoathiriwa na virusi hivyo lakini raia wa Kenya ndio watakayoruhusiwa kurudi nyumbani pamoja na wageni wenye vibali vya kuishi nchini humo, huku shule zote zikifungwa kwa siku 14 zijazo.

Kenyatta amesema watu wawili zaidi walioambukizwa walikuwa na ukaribu na mgojnwa wa kwanza aliyekuwa amerejea nchini humo, baada ya kutokea Marekani na kupitia nchini Uingereza.

Jijini Nairobi, hali hii imezua hali ya wasiwasi na Wakenya wengi wameonekana wakinunua bidhaa mbalimbali kwa hofu kuwa huenda ikawa mbaya zaidi.

Mbali na Kenya, mataifa mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki yaliyoathiriwa na mamabukizi haya ni pamoja na Rwanda, Ethiopia na Sudan.