UFARANSA-UHISPANIA-CORONA-AFYA

Ufaransa na Uhispania zachukua mikakati mipya ya kupambana dhidi ya virusi vya Covid-19

Virusi vya Covid-19 vinaendelea kusababisha vifo duniani, huku vikiendelea kuenea katika nchi mbalimbali.
Virusi vya Covid-19 vinaendelea kusababisha vifo duniani, huku vikiendelea kuenea katika nchi mbalimbali. (Photo By BSIP/UIG Via Getty Images)

Ufaransa na Uhispania zimeungana na Italia kutangaza kusitishwa kwa shughuli za kawaida katika nchi zao, huku Austria ikiwataka raia wote wa kigeni wanaowasili nchini humo kujitenga ikiwa ni mikakati ya kupambana na virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Maambukizi haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa mbalimbami duniani, hasa barani Ulaya, ikiwemo nchi ya Marekani, kupambana na virusi hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 5,800 na wengine 156,000 kuambukizwa.

Mataifa mengi yamepiga marufuku mikusanyiko ya watu na shughuli zingine kama michezo ili kuepuka mikusanyiko ya watu  lakini pia safari za kimataifa kusitishwa.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duiani Papa Francis anatarajiwa kuongoza misa ya pasaka mwezi ujao bila ya kuwepo kwa wauamini wa kanisa hilo katika mji wa Vatican ncini Italia; taifa ambalo limeathiriwa pakubwa baada ya China.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, rais Donald Trump alisema baada ya vipimo hakupatikana na virusi vya Corona,baada ya kukutana na wajumbe kutoka Brazil waliokuwa wameambukizwa virusi hivyo wakati huu akitangaza marufuku zaidi ya safari za ndege kati ya Marekani na nchi za Ulaya.