KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Raia watakiwa kuchukuwa tahadhari Kenya

Wafanyakazi wa afya nchini Kenya wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kujizuia na maambukizi ya virusi vya Covid-19, baada ya kugundua makazi ambapo mgonjwa wa kwanza wa Kenya aliyethibitishwa kupata ugonjwa huo alikuwa akiishi, katika mji wa Rongai.
Wafanyakazi wa afya nchini Kenya wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kujizuia na maambukizi ya virusi vya Covid-19, baada ya kugundua makazi ambapo mgonjwa wa kwanza wa Kenya aliyethibitishwa kupata ugonjwa huo alikuwa akiishi, katika mji wa Rongai. REUTERS/Baz Ratner

Raia nchini Kenya wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona, wakati huu Serikali ikitangaza kufungwa kwa shule na vyuo kama njia ya kudhibiti kuena zaidi kwa maambukizi baada ya watu watatu kuambukizwa.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wataalamu wa afya wanasema licha ya mikakati muhimu iliyotangazwa na Serikali kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, vita ya kuukabili itakuwa ngumu ikiwa wananchi hawataendelea kuelimishwa kuzingatia usafi na njia za kujikinga.

Wakati huo huo wauguzi wanaofanya kazi katika wodi iliyotengwa kwa watu walioambukizwa virusi vya Covid-19 nchini Kenya, wameanza mgomo baridi kulalamikia kile wanachodai kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mafunzo ya kutosha.

Kenya kwa sasa inakabiliwa na kibarua kigumu cha kuwatafuta watu waliotangamana na watu watatu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Covid-19.

Hata hivyo msemaji wa serikali, Cyrus Oguna, ametoa wito kwa watu ambao huenda wa wametangamana na wagonjwa watatu walioambukizwa virusi hivyo kufika katika kituo cha afya kilicho karibu nao.