MAREKANI-CORONA-AFYA

Marekani yafuata nyayo za Ulaya kukabiliana dhidi ya Covid-19

Rais Donald Trump alitaka kuhakikishia raia wake kwa kusema kwamba Marekani inaweza kuzuia janga kubwa la Covid-19 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo, katika Ikulu ya White White, Februari 26, 2020.
Rais Donald Trump alitaka kuhakikishia raia wake kwa kusema kwamba Marekani inaweza kuzuia janga kubwa la Covid-19 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo, katika Ikulu ya White White, Februari 26, 2020. REUTERS/Carlos Barria

Marekani imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao Shirika la Afya Duniani, WHO, liliutangaza kuwa janga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Mikusanyiko ya watu kumi ndio imeruhusiwa nchini Marekani, sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika Jimbo la New Jersey. Pia hatua kadhaa zimechukuliwa kwa maeneo ya miji kama New York, Chicago na Los Angeles.

Marekani inafuata nyayo za nchi kadhaa za Ulaya kwa kuchukuwa hatua kali kwa kukabiliana dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Rais Donald Trump ambaye Jumapili Machi 15 alipiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya hamsini, ameamua kubadili marufuku yake hiyo Jumatatu wiki hii kwa kuweka marufuku kwa mikusanyiko ya watu zaidi ya kumi.

Hatua nyingine zilizochukuliwa, ni pamoja na shule, baa, mikahawa kufungwa, kuepuka safari zisizo za muhimu.

Hatua hizi zilitangawa kupitia njia ya vidio katika mkutano na wakuu wa majimbo ya Marekani.

Hapo awali Gavana wa Jimbo la New York, ambaye ni kutoka chama cha Democratic, moja ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na janga hilo, alimkosoa rais wa Donald Trump kwa "kushindwa kuchukua maazimio yaliyo wazi".

"Kuna wimbi la hatua zilizochukuliwa nchini kote - ni hatari," amesema Gavana wa wa Jimbo la New York, Andrew Cuomo, ambaye ni mpinzani wa kisiasa wa rais Trump.

Wakati kesi za maambukizi zilizothibitishwa nchini Marekani zinakaribia watu 4,300 - ikiwa ni pamoja na vifo zaidi ya 74 - New Jimbo la Jersey, jirani na New York, pia ni jimbo la kwanza nchini Marekani kutangaza Jumatatu wiki hii sheria ya kutotoka nje usiku (baada ya eneo la Porto Rico).

"Kuanzia usiku wa leo, biashara zote na shughuli za burudani zisizo za muhimu zitafungwa saa mbili usiku," Gavana Phil Murphy ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

"Usafiri wowote usio wa muhimu (...) umepigwa marufuku kati ya saa mbili usiku na saa kumi na moja alfajiri, " Gavana Phil Murphy ameongeza.

Janga la Covid-19 linaendelea kuzua hofu duniani, maambukizi ya ugonjwa huo yanaendelea kuripotiwa katika nchi mbalimbali duniani.