NEW-ZEALAND-CORONA-AFYA

Coronavirus: Wageni marufuku kuingia New Zealand

Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa New Zealand, akizungumza kupitia televisheni.
Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa New Zealand, akizungumza kupitia televisheni. Reuters

New Zealand imeaumu kufunga mipaka yake kwa raia wote wa kigeni, uamuzi liyochukuliwa leo Alhamisi kama sehemu ya hatua kali za kupambana dhidi ya kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covi-19 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu, Jacinda Ardern amesema raia wa New Zealand na raia wa kigeni ambao wana kibali cha kuishi nchini humo ndio pekee waoweza kuingia nchini.

Hata hivyo amebaini kwamba kwa raia hao aliotaja itakuwa vigumu kurejea nchini kutokana na kwamba mashirika mengi ya ndege yamefuta safari katika nchi kadhaa duniani.

"Hatutavumilia hatari yoyote katika mipaka yetu," Ardern amesema.

Mipaka inabaki wazi kwa mizigo na biashara, ameongeza.

Nchini New Zealand kunaripotiwa kesi 28 za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.