DRC-CORONA-AFYA

DRC: Tshisekedi atangaza hatua dhidi ya Covid-19

Felix Tshisekedi katika hafla ya kuapishwa Januari 24, 2019 huko Kinshasa
Felix Tshisekedi katika hafla ya kuapishwa Januari 24, 2019 huko Kinshasa TONY KARUMBA / AFP

Jamhuri ya Kidemokrasia ay Congo imetangaza visa 14 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 nchini humo. Rais wa DRC Félix Tshisekedi ametangaza hatua za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo, ambao shirika la Afya Duniani, WHO, liliuita kuwa ni janga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Daktari Jean-Jacques Muyembe, mratibu wa mapambano dhidi ya virusi vya Ebola, sasa ni mratibu wa mapambano dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

"Tuko mwanzoni mwa janga hili. Ugonjwa huu ni tishio kubwa ambalo linataka hatua kali, "rais Felix Tshisekedi amesema katika ujumbe wake.

Hatua hizo zilizotangazwa, zinafanana na zile ambazo tayari zimeanza kutumika katika nchi nyingi duniani.

► Soma pia: Coronavirus: Nchi za Afrika zaendelea kukabiliana na kusambaa kwa virusi

Mikusanyiko yote, mikutano, sherehe za watu zaidi ya ishirini kwenye maeneo ya umma ni marufuku nchini kote DRC. Shule na vyuo vikuu vimefungwa kwa mwezi mmoja kuanzia leo Alhamisi.

Sherehe zote za ibada ya watu wengi na michezo katika viwanja mbalimbali na sehemu zingine za mikusanyiko pia zimepigwa marufuku. Sherehe zote za starehe, baa, mikahawa vimefungwa. Aina zingine za mikusanyiko, kama misiba imewekwa chini ya kanuni maalum, "watu hawaruhusiwi kukusanyika nyumbani kwa marehemu au sehemu yoyote ile", "mwili unachukuliwa moja kwa moja kutoka chumba cha kuhifadhi maiti kwenda mahali pa mazishi kwa idadi ndogo ya watu wanaoshindikiza jeneza" , amesema wa DRC.

Félix Tshisekedi pia "amechukua uamuzi wa kusitisha safari zote za ndege kutoka nchi zilizoatghirika na ugonjwa wa Covid-19".