CAMEROON-CORONA-AFYA

Coronavirus: Cameroon kuendelea na biashara yake ya mipakani

Bandari ya Douala huko Cameroon.
Bandari ya Douala huko Cameroon. Reinnier KAZE/AFP

Licha ya kitisho cha ugonjwa hatari wa Covid-19 Cameroon imeapa kuendelea na biashara yake na nchi za CEMAC, mamlaka ya Cameroon imetangaza Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, katika vita dhidi ya Covid-19, Waziri Mkuu alitangaza kufungwa kwa "mipaka ya ardhini,angani, na mipaka ya baharini" ya nchi hiyo isipokuwa kwa "ndege za mizigo" na "meli zinazobeba bidhaa mahitajio" na" bidhaa muhimu ", bila maelezo zaidi kuhusu magari ya mizigo, hali ambayo imezua sintofahamu katika nchi jirani, zinazotegemea biashara hizo kwa maisha yao ya kila siku.

Jumatano wiki hii, Waziri Mkuu alisema kwamba biashara ya mpakani itaendelea, "hasa na Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati".

Hata hivyo jana Alhamisi, serikali ya Cameroon ilitoa tangazo jipya la kuondoa mtafaruku uliopo: Cameroon itaendelea na biashara yake na "nchi zote za CEMAC", ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad, lakini pia Gabon, Congo na Equatorial Guinea.

Ikumbukwe kwamba Cameroon ni moja wapo ya nguzo muhimu katika biashara katika jumuiya hiyo. Asilimia 24.7 pekee kati ya mwaka 2014 na 2017, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kuhusu matarajio ya kiuchumi barani Afrika, "kutokana na uwepo wa barabara inayounganisha nchi zote za CEMAC na Nigeria". Bandari ya Douala pia ni lango kuu la bidhaa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad. Asilimia 80 ya bidhaa vinavyoingia na kutoka Chad zipitia Cameroon.