MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marekani yashauri raia wake wasifanyi safari za nje

Marekani yaendelea na vita dhidi ya janga la Covid-19 na kuwataka raia wake kuchukuwa tahadhari.
Marekani yaendelea na vita dhidi ya janga la Covid-19 na kuwataka raia wake kuchukuwa tahadhari. REUTERS

Marekani imewataka raia wake wote kutofanya safari za nje ya nchi kwa sababu ya janga la Covid-19 na kushauri wale ambao wako nje ya nchi warudi haraka iwezekanavyo.

Matangazo ya kibiashara

"Mkichagua kusafiri nje ya nchi, mipango yenu ya kusafiri inaweza kukwama nje ya nchi na unaweza kulazimika kubaki nje ya Marekani kwa muda usiojulikana," Wozara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema katika taarifa.

"Katika nchi mbalimbali viwanja vya ndege vimefungwa. Raia wa Marekani almbao wanaishi nje ya nchi wanaweza kujipanga kwa kurudi mara moja nchini Marekani, la sivyo wataendelea kubaki nje ya nchi kwa muda usiojulikana" , Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imeongeza.

Mamlaka haitoi tena visa yoyote isipokuwa kwa "dharura za maisha na kifo".

Balozi wa Marekani nchini Morocco David Fischer katika video aliyorusha kwenye ukurasa wake wa Twitter amebaini kwamba ubalozi wa Marekani jijini Rabat na Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani wanafanya kazi "saa 24 kwa siku" ili raia wote wa Marekani wanaohitaji kurudi nyumbani waweza kurudi salama.