ISRAELI-PALESTINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Eneo lote la Msikiti wa Alqsa Jerusalem kufungwa kwa waumini

Msikuti wa Alqsa huko Jérusalem.
Msikuti wa Alqsa huko Jérusalem. REUTERS/Eliana Aponte/File Photo

Eneo la Msikiti wa Alqsa huko Jerusalem litafungwa kwa umma kuanzia Jumatatu wiki hii ili kuzuia kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kipekee imetangazwa na Waqf, taasisi inayosimamia maeneo matakatifu ya Waislam katika mji mtukufu wa Jerusalem.

Ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 1967 eneo hilo la tatu la Uislamu kufungwa kwa waumini kwa uamuzi wa Waqf, mkurugenzi wa msikiti wa Al-Aqsa, Sheikh Omar Al-Kisswan, ameliambia shirika la Habari la AFP.

Israeli, ambayo vikosi vyake vinadhibiti barabara zote za kuingia kwenye maeneo ya Msikiti wa Alqsa, iliwahi kufunga msikiti huyo katika miaka ya hivi karibuni baada ya kutokea vurugu.

Kulingana na taarifa ya Waqf ya Jumapili, waumini hawataweza kwenda kwenye Mskiti wa Alqsa "kwa kipindi cha muda mfupi kufuatia mapendekezo ya kidini na ya kimatibabu". Wafanyakazi pekee ndio wanaruhusiwa na watafanya ibada zao nje ya msikiti, taarifa hiyo imeongeza.