MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Marekani yaandaa mpango kabambe wa kusaidia uchumi

Marekani itatoa Dola Trilioni 4 kusaidia makampuni ili waweze kuendelea kulipa wafanyakazi wao, lakini pia yawe tayari kuendelea na shughuli wakati hali itarudi kuwa sawa
Marekani itatoa Dola Trilioni 4 kusaidia makampuni ili waweze kuendelea kulipa wafanyakazi wao, lakini pia yawe tayari kuendelea na shughuli wakati hali itarudi kuwa sawa CC0 PIxabay/geralt

Marekani inaandaa mpango kabambe wa kusaidia uchumi wake ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao shirika la Afya Duniani liliutaja hivi karibuni kuwa ni janga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ambayo ni nchi ya kwanza yenye uchumi mkubwa duniani inasema iko tayari kutoa Dola Trilioni 4 ili kusaidia makampuni mbalimbali.

Sekta mbalimbali zimeathirika nchini Marekani kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona. Ili kusaidia makampuni hayo kujinasua kiuchumi, lazima yasaidiwe kifedha, Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, amesema katika mahojiano na Fox News.

"Hali inabadilika haraka," amesema. Tunahitaji kuweka pesa kwenye uchumi mara moja. Ikiwa tutafanya hivyo, tunaweza kuleta utulivu kwa uchumi. Pia tunatoa pesa nyingi katika hospitali. Rais anatarajia yote haya kuwezekana ndani ya kipindi cha wiki nne zijazo. "

Waziri wa Fedha wa Marekani bado ana matumaini, lakini anasema bado kazi ni kubwa: Dola Trilioni 4 zitatolewa. Hii ni kusaidia makampuni ili yaendelea kulipa wafanyikazi wao, lakini pia yawe tayari kuendelea na shughuli wakati hali itarudi kuwa sawa.

Taasisi ya kitaifa pia itatumika na kutoa mikopo kwa makampuni madogo madogo. Katika mpango huo kuna fedha ambazo zimeandaliwa kwa hospitali. Familia za Wamarekani zitapokea Dola 1,000 kwa kila mtu mzima na Dola 500 kwa kila mtoto.