MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Mpango wa kuinua uchumi wakwama Marekani

Baraza la Congress lakwamisha mpango wa kufufua kuinua uchumi wakati nchi hii inaendelea kukumbwa na mgogoro wa wakiafya kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Baraza la Congress lakwamisha mpango wa kufufua kuinua uchumi wakati nchi hii inaendelea kukumbwa na mgogoro wa wakiafya kutokana na ugonjwa wa Covid-19. NICHOLAS KAMM / AFP

Mpango wa kuinua uchumi wa Marekani umekwama bungeni baada ya wabunge kutoka chama cha Republican na wale kutoka chama cha Democratic kushindwa kuelewana.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ilikuwa inaandaa mpango kabambe wa kuinua uchumi wake ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao shirika la Afya Duniani liliutaja hivi karibuni kuwa ni janga la kimataifa.

Marekani ambayo ni nchi ya kwanza yenye uchumi mkubwa duniani inasema iko tayari kutoa Dola Trilioni 2 ili kusaidia makampuni mbalimbali.

Wabunge kutoka chama cha Republican na wale kutoka chama cha Democratic hawakuweza kukubaliana juu ya muswada ambao utachukuwa Dola Trilioni 2.

Kwa mujibu wa wabunge kutoka chama cha Democratic mpango huo utanufaisha tu makampuni kuliko wafanyakazi.

Mazungumzo yanaendelea katika faragha wakati mgogoro wa kiafya unazidi kuongezeka kwa kiasi kwamba ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kushika kasi.

Siku tatu za mazungumzo makubwa hazikuweza kutosha kufikia makubaliano. Licha ya changamoto nyingi, mpango wa kufufua uchumi, jambo muhimu zaidi katika historia ya Marekani, haukuleta ushawishi wowote.