MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Serikali ya Mexico kufunga maeneo ya kitamaduni na ya kitalii

Wiki iliyopita Mexico iliafikiana na Marekani kufunga mpaka wa nchi hizo mbili kuzuia kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Wiki iliyopita Mexico iliafikiana na Marekani kufunga mpaka wa nchi hizo mbili kuzuia kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19. REUTERS/Lucy Nicholson

Serikali ya Mexico imeamua kufunga maeneo ya kitamaduni na ya kitalii, hatua ambayo itaanza kutumika Jumatatu hii Mars 23 kote nchini.Ni hatua ya kwanza inayochukuliwa na serikali ya Mexico tangu kufikiwa kwa makubaliano wiki iliyopita na Marekani kuhusu kufunga mpaka.

Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumatatu hii, maeneo ya kitamaduni na ya kitalii pamoja na nyumba za sinema nchini zitafungwa.

Hatua hiyo imechukuliwa katika hali ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambapo watu wawaili wamefariki dunia kutokana na mlipuko huo, huku watu 300 wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ambao shirika la Afya Duniani, WHO, liliuita janga la kimataifa.

Serikali ya Mexico ni moja ya serikali kuchukuwa hatua dhidi ya ugonjwa huo katika ukanda wa Kusini mwa Amerika na raia wameendelea kuwa na hofu kuwa kesi za maambukizi na vifo kuenda vikaongezeka.

Mji wa Mexico tayari umechukua hatua kama vile kufunga baadhi ya maeneo ya umma (baa, ntyumba na kumbi za shtarehe) ili kulinda wakazi wake milioni 9. Vivyo hivyo, mechi za ligi ya mpira wa miguu zimesitishwa na baadhi ya kampuni zimechukua hatua ya kuwataka wafanyakazi wao kukaa nyumbani.