MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Bunge la Seneti la Marekani lapanga kupigia kura mpango wa kuinua uchumi

Nchini Marekani Baraza la Congresslimezuia mpango wa kuinua uchumi wakati nchi hii inapitia mgiogoro wa corona.
Nchini Marekani Baraza la Congresslimezuia mpango wa kuinua uchumi wakati nchi hii inapitia mgiogoro wa corona. NICHOLAS KAMM / AFP

Bunge la Seneti la Marekani linaweza kupitisha mpango wa kuinua uchumi wa Marekani wa dola bilioni 2000 (sawa na euro bilioni 1.842) katika kukabiliana na janga la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa chama cha Republican na wale wa chama cha Democratic wamepiga hatua muhimu katika mazungumzo yao.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, ametangaza kwamba atarudi Kapitol Jumanne wiki hii baada ya siku moja ya mazungumzo yaliyomalizika Jumatatu saa sita usiku bila makubaliano.

Steven Mnuchin, ambaye amesema alifanya mazugumzo angalau mara 10 na rais Donald Trump wakati wa majadiliano ya kasi Jumatatu wiki hii, na Chuck Schumer, kiongozi wa kundi la maseneta kutoka chama cha Democratic, hawakutoa maelezo kuhusu maendeleo ya mazungumzo hayo, lakini wote wawili walikuwa na matumaini.