G20-CORONA-AFYA

Coronavirus: Mkutano wa dharura wa G20 kufanyika Alhamisi

Katika hali ya kupambana dhidi ya janga la Covid-19, maafisa wa polisi wa DRc wapiga doriua katika mitaaa ya jiji la Goma, mashariki mwa DRC, Machi 19, 2020.
Katika hali ya kupambana dhidi ya janga la Covid-19, maafisa wa polisi wa DRc wapiga doriua katika mitaaa ya jiji la Goma, mashariki mwa DRC, Machi 19, 2020. REUTERS/Olivia Acland

Viongozi wa nchi zilizostawi kiviwanda na kiuchumi, G20, wanatarajia kukutana kwa mazungumzo kupitia video Alhamisi wiki hii kuhusu janga la kimataifa la Covid-19, kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, likinukuu vyanzo kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unakuja wakati viongozi kadhaa duniani wanalaumu kundi hilo la nchi zilizostawi kiviwanda na kiuchumi, G20, kwa kujikokota katika kukabiliana na madhara ya kiuchumi yanayosababishwa na ugonjwa huo hatari duniani.

Mawaziri wa fedha wa G20 na viongozi wa mabenki kuu kutoka nchi hizo waliahidi Jumatatu wiki hii katika mkutano kupitia video kuendeleza "mpango wa hatua" kukabiliana na janga hilo, kulingana na Shirika la fedha duniani, IMF, litasababisha kushuka kwa uchumi duniani.

Mkutano wa kilele wa Alhamisi utafanyika wakati kukiripotiwa vita vya bei ya mafuta kati ya nchi mbili wanachama wa G20, Saudi Arabia na Urusi, na mvutano kati ya wanachama wengine, Marekani na China, kuhusu chanzo cha janga hilo ambalo limesababisha vifo zaidi ya 16,500 na visa 378,000 vya maambukizi.