UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi 4,700 za maambukizi na vifo vipya 28 vyaripotiwa Ujerumani

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, Berlin, Ujerumani, Februari 27, 2020.
Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, Berlin, Ujerumani, Februari 27, 2020. REUTERS/Annegret Hilse

Ujerumani inaendelea kukumbwa na ongezeko la visa vya mambukizi ya virusi vinavyosababisha na ugonjwa wa Covid-19, huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Ujerumani imetangaza kesi 27,436 za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (Covid-19), huku visa vipya 4,764 vikiripotiwa leo Jumanne, kulingana ripoti ya taasisi Robert Koch, mamlaka ya afya nchini Ujerumani.

Idadi ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo hatari wa Covid-19 imefikia 114, 28, huku vifo vipya 28 vikiripotiwa kutokea usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Ujerumani inaweza kupoteza karibu Dola Bilioni 538 (sawa na Euro Bilioni 500) katika madhara ya mripuko wa virusi vya Corona na kufungwa kwa sehemu kwa shughuli za kimaisha.

Wakati huo huo msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Steffen Seibert amesema majibu ya vipimo vya virusi vya Corona yametoka na kuonyesha kuwa kiongozi huyo yuko salama, kulingana na shirika la habari la Ujerumani dpa.

"Matokeo ya vipimo vya leo yameonyesha kuwa Kansela Angela Merkel hana mambukizi yoyote, " amesema Steffen Seibert, huku akibaini kwamba vipimo zaidi vitafanyika katika siku zijazo."

Angela Merkel alijiweka karantini nyumbani siku ya Jumapili jioni baada ya kufahamishwa kwamba daktari aliempatia chanjo alikutwa na virusi vya corona.