CAMEROON-DIBANGO-CORONA-AFYA

Mwanamuziki mkongwe wa Cameroon Manu Dibango afariki dunia kwa virusi vya Covid-19

Manu Dibango katika studio za RFI, Septemba 27, 2019.
Manu Dibango katika studio za RFI, Septemba 27, 2019. RFI/Anthony Ravera

Mwanamuziki na mpiga talumbeta wa Cameroon Manu Dibango ambaye alivunja rekodi kwenye soko la muziki huko Amerika mnamo 1973 na kibao chake cha 'Soul Makossa', amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 kutokana na ugonjwa wa Covid-19 (Corona).

Matangazo ya kibiashara

Manu Dibango alikuwa amelazwa hospitalini kwa siku kadhaa, baada ya kupimwa na kupatiana na virusi voinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Manu Dibango alikuwa amelazwa hospitalini kwa siku kadhaa, baada ya kupimwa na kupatiana na virusi voinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Manu Dibango alidhamiria sana kwenye muziki. Manu Dibango ambaye alizaliwa nchini Cameroon mnamo mwaka 1933, alifariki dunia akiwa nje ya hospitali, jijini Paris, nchini Ufaransa.

Wiki iliyopita N'djoke Dibango ' Manu Dibango' kwenye ukurasa wake wa Facebook, alitangaza kupatwa na ugonjwa wa virusi vya Covid-19 (Corona).

Hii hapa ni moja ya nyimbo zake zilizopendwa 'Soul Makossa'