AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Watu 402 waambukizwa virusi vya Covid-19 Afrika Kusini

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya zaidi ya nusu ya visa vilivyotokea Afrika Kusini vimepatikana katika jimbo la Gauteng, linalolijumisha jiji la Johannesburg.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya zaidi ya nusu ya visa vilivyotokea Afrika Kusini vimepatikana katika jimbo la Gauteng, linalolijumisha jiji la Johannesburg. Guillem Sartorio / AFP

Afrika Kusini inaendelea kukumbwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-, ambao shiorika la Afya Duniani liliutaja kuwa ni janga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa Afrika Kusini, moja ya nchi zinazoendelea kuwa na visa vingi vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo barani Afrika, wana hofu kuwa idadi uya visa vya maambukizi ikaondelea kuongezeka na kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Wasafiri kutoka Ulaya na mataifa mengine ndio wanaripotiwa kuwa wengi kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Afrika Kusini, ingawa idadi ya maambukizi ya ndani pia inaongezeka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya zaidi ya nusu ya visa vilivyotokea Afrika Kusini vimepatikana katika jimbo la Gauteng, linalolijumisha jiji la Johannesburg, ambalo ni kubwa kabisa nchini humo lenye idadi ya watu milioni 5.7, na mji mkuu Pretoria ambao una watu milioni 2.4.

Afrika Kusini sasa inaongoza dhidi ya Misri kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ingawa bado hakujaripotiwa kifo.