MADAGASCAR-CORONA-AFYA

Coronavirus Madagascar: Raia watakiwa kuzingatia hatua za kusalia nyumbani

Eneo lenye watu wengi la Anjanahary II N, Antananarivo. (picha ya kumbukumbu)
Eneo lenye watu wengi la Anjanahary II N, Antananarivo. (picha ya kumbukumbu) Laetitia Bezain/RFI

Kutokana na kukosekana kwa misaada, hali ya maisha kwa mamia ya maelfu ya wakaazi wa mji mkuu wa Madagascar, imekuwa ngumu, huku utekelezaji wa hatua za kukaa nyumbani ukiambulia pa tupu.

Matangazo ya kibiashara

Pia, katika mji mkuu Antananarivo, vitengo mbalimbali vya polisi vinaendelea kupiga doria mchana na usiku ili kuwazuia watu wasitoke majumbani kwao.

"Hakuna mtu anayetakiwa kuwa barabarani, watu wote wanatakiwa kuondoka maeneo haya na kwenda nyumbani!" », polisi imesema kupitia vipaza sauti.

Jumanne alasiri, mji mkuu wa Madagascar ulikuwa patupu, huku shughuli nyingi zikizorota, ispokuwa tu watembea kwa miguu ndio wameonekana katika mitaa mbalimbali ya mji huo hadi saa sita mchana.

"Ni vigumu kudhibiti hali hii ya kuwazuia raia hawa maskini zaidi. Kwa sababu tunajua kuwa ikiwa wako nje, ni kutaka wapate chakula watachokula jioni. Kwa hivyo hali hii ni ngumu ukilinganisha na kazi ambayo tumepewa. Lakini bado tunajaribu kuwashawishi wasitoke, " afisa mmoja wa polisi amabye hakutaka kutaja jina lake amebaini

Wakati huo huo serikali imeunda timu zinazojumuishwa na madaktari na polisi, ambao jukumu lao kubwa ni kukaguwa na kupima watu ambao wamerudi hivi karibuni kutoka nje ya nchi na ambao wamewekwa karantini, katika hoteli na katika maeneo mengine.