MALI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa viwili vya maambukizi vyathibitishwa Mali

Mtafiti kutoka Mali anayehusika na kuchunguza sampuli ya damu ili kujua kama ina ugonjwa wa Covid-19, Bamako, Machi 19, 2020.
Mtafiti kutoka Mali anayehusika na kuchunguza sampuli ya damu ili kujua kama ina ugonjwa wa Covid-19, Bamako, Machi 19, 2020. AFP Photos/Michele Cattani

Mali imetangaza visa viwili vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona) nchini humo, wakati nchi hii ilikua haijaripoti kisa chochote cha maambukizi tangu ugonjwa huo kuzuka mnamo mwezi Desemba 2019.

Matangazo ya kibiashara

Wagonjwa wote ni raia wa Mali, mwanamke mmoja, mwenye umri wamiaka 49 kutoka mji wa Bamako na mwanaume mmoja, mwenye umri wa miaka 62, kutoka mji wa Kayes (ukanda wa Magharibi mwa Mali).

Wote wawili waliwasili nchini Mali kutoka Ufaransa Machi 12 na 16, 2020.

Mara baada tu ya kesi hizo kugunduliwa, wagonjwa hao wawili wanahudumiwa na mamlaka ya afya nchini Mali, Waziri wa Afya, Michel Sidibé, amebainisha.

"Wagonjwa hao wawili wawanaendelea kupata matibabu kutoka kwa mamlaka ya afya, " amesema waziri wa afya. Mali ilikuwa nchi adimu katika bara la Afrika kutokuwa na kesi yoyote ya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Serikali ya Mali imeandaa bahasha ya kwanza ya faranga takriban bilioni 6 za CFA katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19. Na msaada umeombwa washirika wa kigeni.