UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi 31,000 za maambukizi na vifo 149 vyathibitishwa Ujerumani

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri watu wengi duniani.
Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri watu wengi duniani. AFP

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 imeongezeka hadi 31,554 nchini Ujerumani, ambapo watu 149 wamefariki dunia, imetangaza taasisi ya Robert-Koch, mamlaka ya afya nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hii inaoyesha kesi mpya 4,191 za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 na vifo vipya 36 ukilinganisha na ripoti iliyopita.

Virusi vya Corona (Covid-19) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.

Virusi hivyo ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.