UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi 36,000 za maambukizi na vifo karibu 200 vyathibitishwa Ujerumani

Ujerumani imetangaza karibu kesi mpya 5,000 za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona) idadi ya vifo imeongezeka kwa theluthi moja na kufikia 198, Taasisi ya Robert Koch, mamlaka ya afya nchini humo imesema leo Alhamisi.

Ujerumani inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19 (Corona).
Ujerumani inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19 (Corona). © Reuters / Matthias Rietschel
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 nchini Ujerumani sasa imefikia 36,508, sawa na kesi mpya zaidi ya 4,995 siku moja iliyopita.

Virusi vya Corona (Covid-19) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.

Virusi hivyo ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.