UFARANSA-CORONA-AFYA

Macron aandaa 'mpango muhimu' baada ya 'mazungumzo mazuri' na Trump

“Pamoja na nchi zingine, tunajiandaa kwa siku chache zijazo mpango mpya muhimu," ametangaza rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
“Pamoja na nchi zingine, tunajiandaa kwa siku chache zijazo mpango mpya muhimu," ametangaza rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa kuwa amezungumza na mwenzake wa Marekani, Donald Trump juu ya suala la janga ya Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

“Pamoja na nchi zingine, tunajiandaa kwa siku chache zijazo mpango mpya muhimu," ametangaza rais wa Ufaransa katika ujumbe uliochapishwa kwa lugha ya Kifaransa na kisha kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Twitter.

Janga hili kuanzia kuskazini hadi kusini, Mashariki na Magharibi mwa dunia ni tishio la Covid-19. Kwa wastani maambukizi haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa yote duniani, hasa Marekani na barani Ulaya na mipaka yake yote.

Kwa sasa nchini Italia imefunga na kusimamisha shughuli katika bandari zake katika hali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Wizara ya uchukuzi imeziagiza meli ambazo tayari ziko baharini kurudi bandarini na watu wote kufanyiwa vipimo.

Hata hivyo Nchini Uingereza pia imewaomba madaktari wastaafu kurudi kazini ili kusaidia kukabiliana na janga la Corona. Baraza la wauguzi na wakunga nchini Uingereza limewaandikia barua zaidi ya wauguzi 50,000 pamoja na madaktari 15,000 waliostaafu ili kurudi kazini kwa ajili ya kusaidia kupambana na janga la virusi vya Corona. Suala hili pia la kuwarudisha wakunga na madaktari wastaafu limefanyika nchini Italia hata wauguzi na madaktari wapya ambao walikuwa hawajapata ajira na zaidi ambao wamepata shahada hivi karibuni, wote wamealikwa kushiriki kusaidia dharura hii. Kufuatia na janga hili Waziri mkuu wa Italia Bwana Conti ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutumia uwezo wake imara wa kifedha katika kupambana na janga la Corona.

Jiji la Madrid, ni kitovu cha janga nchini Hispania na hivyo wamezindua , programu ya kutathmini dalili zake.Uhispania zimeungana na Italia kutangaza kusitishwa kwa shughuli za kawaida katika nchi zao, huku Austria ikiwataka raia wote wa kigeni wanaowasili nchini humo kujitenga ikiwa ni mikakati ya kupambana na virusi vya Corona. Kwa wastani maambukizi haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa mbalimbami duniani, hasa barani Ulaya na mipaka yake yote.

Hivi karibuni Korea Kusini ilitangaza kwamba visa vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 vimeongezeka, baada ya kupungua kwa visa vilivyothibitishwa siku kadhaa zilizopita. Hali hiyo inajiri wakati mlipuko mpya wa janga hilo umeonekana katika kituo cha kuwahudumia watu waliostaafu huko Daegu, mji wa Kusini mwa Korea Kusini, ulioathirika zaidi na virusi hivyo.

Marekani, ambayo maambukizi ya virusi hivyo yamezidi mara dufu na sheria ya kuwalazimisha watu wakae nyumbani ndiyo inaendelea kutolewa. Kando na Jiji la New York na Washington, California ni miongoni mwa majimbo yaliyozongwa na janga la Covid-19.

Afrika Kusini, kama nchi nyingine kuwa na maambukizi ya virusi na hivyo serikali kutangza marufuku ya kutotoka nje kwa raia wote wa nchi hiyo. Hivi karibuni rais Cyrille Ramaphosa alitangaza kusitishwa kwa safari kutokea katika mataifa yenye tishio kubwa la Covid-19 kama Italia , Ujerumani, China na Marekani. Vile vile mtu yeyote ambaye ataeneza habari za uwongo kuhusu ugonjwa wa Covid-19 sasa atakabiliwa na adhabu kubwa ya miezi sita gerezani, kulingana na sheria mpya.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika Mkoa wa Hubei, nchini China.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.