UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi nchini Ujerumani yafikia 57,298 na vifo 455

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini Ujerumani imefikia 57,298, huku vifo vikipindukia 455, kwa mujibu wa data za taasisi ya udhibiti wa magonjwa, Robert Koch.

Ndege ya kijeshi ya Ujerumani ikiwachukua wagonjwa wa walio ambukizwa Covid-19 huko Strasbourg (Ufaransa) na kuwahamishia huko Ulm (Ujerumani). Machi 29, 2020.
Ndege ya kijeshi ya Ujerumani ikiwachukua wagonjwa wa walio ambukizwa Covid-19 huko Strasbourg (Ufaransa) na kuwahamishia huko Ulm (Ujerumani). Machi 29, 2020. Luftwaffe/Johannes Heyn/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii inaonyesha visa vipya 4,751 vya maambukizi na vifo vipya zaidi ya 66 ikinganishwa na ripoti ya siku moja iliyopita, kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters.

Kwa sasa serikali ya Ujermani imechukua mikakati ya kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo: kuzidisha vipimo na kuwaweka wagonjwa karantini.

Hata hivyo baadhi ya hospitali nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi.

Mwanzoni mwa mwezi Machi maonyesho kadhaa yaliahirishwa ikiwemo maonyesho ya Utalii ya Berlin ITB, maonyesha ya viwanda ya Hannover na yale ya vitabu ya mjini Leipizig.

Hivi karubuni Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn, alisema walitangaza hatua za kuimarisha uchumi unaonekana kutetereka kutokana na kuenea kwa mripuko wa virusi vya Corona wakati pia wakiyazuia matukio yote makubwa yaliyopangwa kufanyika.

Ujerumani ni mojawapo ya nchi za Ulaya ambazo zinaendelea kuathirika na ugonjwa huu hatari wa Covid-19, ambao shirika la Afya Duniani; WHO, liliutangaza kuwa ni janga la kimataifa.