JAPAN-CORONA-AFYA

Coronavirus: Michezo ya Olimpiki ya Tokyo kufunguliwa Julai 23, 2021

Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, iliyoahirishwa kwa sababu ya janga la sasa la Corona, itafunguliwa Ijumaa Julai 23, 2021. Michezo hiyo itafunguliwa mwaka mmoja baada ya tarehe iliyokuwa imepangwa hapo awali.

Michezo ya Olimpiki itaanza Julai 23, 2021 na itamalizika Agosti 8, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Japani, Yoshiro Mori, ametangaza
Michezo ya Olimpiki itaanza Julai 23, 2021 na itamalizika Agosti 8, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Japani, Yoshiro Mori, ametangaza REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki (IOC) ilikuwa imeitisha mkutano wa baraza lake kuu kuhusu tarehe mpya za Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, Jumatatu Machi 30.

Tume hiyo ilitangaza, Jumanne iliyopita, kuwa michezo hiyo imeahirishwa hadi mwaka 2021. Ilikuwa inasubiriwa tu tarehe ya ufunguzi wa michezo hiyo.

Michezo ya Olimpiki itaanza Julai 23, 2021 na itamalizika Agosti 8, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Japani, Yoshiro Mori, ametangaza leo Jumatatu mchana. Baada ya kushauriana siku ya Alhamisi na mashirikisho yote 33 ya kimataifa ya michezo yanayoshiriki michezo hiyo ya olimpiki, siku iliyofuata Kamati za Kitaifa za Olimpiki, IOC ziliafikiana kuhusu tarehe hizo.

Michezo ya wanariadha walemavu itaanzia Agosti 24 hadi Septemba 5, pia ametangaza Yoshiro Mori.