Coronavirus: Wafanyakazi katika hospitali mbalimbali DRC walalamikia uhaba wa vifaa
Kutekeleza marufuku ya kutotoka nje au la? Hiyo ndio hali inayojiri jijini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wakazi wa mji huo wanaendelea kuishi kwa wasiwasi.
Imechapishwa:
Wiki iliyopita, Gavana wa mji mkuu wa DRC alitangaza hatua ya kutotoka nje kabla ya kuifuta bila maelezo yoyote. Ikumbukwe kwamba tangazo hilo lilizua sintofahamu: wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu walilaani hatua hiyo na kubaini kwamba serikali haina mtazamo wowote katika mkakati unaoweza kupitishwa kwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Hata hivyo wakazi wa mikoa mingine jirani ya Kishasa wanasema wana hofu ya kuenea kwa ugonjwa huo hatari.
Wakati huo huo visa viwili vya kwanza vya maambukizi ya virusi vya Corona, vimeripotiwa jijini Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini na kuwa na mkoa wa tatu kuathiriwa na maambukizi hayo baada ya Kinshasa na Ituri.
Hayo yanajiri wakati wafanyakazi wa afya wanaomba wapatishiwe uwezo na vifaa vya kutosha kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.