DRC-CORONA-AFYA

DRC: Mijadala yaibuka kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na Corona Kinshasa

Bado hakujachukuliwa uamuzi wa wa kukaa nyumbani katika mji wa Kinshasa, DRC.
Bado hakujachukuliwa uamuzi wa wa kukaa nyumbani katika mji wa Kinshasa, DRC. REUTERS/Robert Carrubba/File Photo

Baada ya serikali kutangaza hatua ya kutotoka nje katika mji wa Kinshasa na baadae kufutwa, wakazi wa mji huo wanaendelea kusubiri hatua mpya dhidi ya janga la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi waendelea kukutana ili kuamua hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Siku ya Jumapili hii, Rais Félix Tshisekedi alikutana tena na kamati ya mseto ili ujadili hasa hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

"Katika hatua hii, mambo yote yako mezani," chanzo kilio karibu na ofisi ya rais kimesema. Maoni yote yalitolewa na wataalamu mbali mbali kutoka manispaa ya jiji la Kinshasa, ofisi ya Waziri Mkuu na wasaidizi wa rais wa Jamhuri.

Wengine wanapendekeza marufuku ya kutoka nje kwa baadhi ya maeneo, hatua ambayo itahusu Wilaya ya Gombe pekee, kituo cha biashara cha mji mkuu wa DRC. Watetezi wa msimamo huu wanatoa hoja yao kwamba kesi nyingi za maambukizi zilizothibitishwa ziliripotiwa katika sehemu hiyo ya jiji. Hii pia ilipendekezwa wakati wa mkutano wa kimkakati na Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba wiki iliyopita.

Uamuzi watarajiwa Jumanne hii

Hoja hii inafutiliwa mbali kabisa na wataalam wengine, hasa katika ngazi ya serikali ya mkoa wa Kinshasa, ambao wanaeleza kuwa watu wengi ambao wapo wilayani Gombe hutokea katika wilaya zingine za mji mkuu. Wataalamu haoa wanasema, hatua ya kubaki nyumbani italenga jiji lote la Kinshasa kwa siku kadhaa.

Kwa upande wake, Jean-Jacques Muyembe, mkuu wa idara inayokabiliana na ugonjwa huo, amesema Jumanne hii asubuhi kwamba bado ni mapema sana kuamua juu ya mfumo wa marufuku hiyo. "Mambo yanaweza kuwa sawa baadae Jumanne hii jioni," amesema.