ASIA-WHO-CORONA-AFYA

WHO: Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kwa kasi katika ukanda wa Asia

Shirika la Afya Duniani limezitaka nchi zote kuazisha mipango yao ya maamdalizi dhidi ya janga Corona.
Shirika la Afya Duniani limezitaka nchi zote kuazisha mipango yao ya maamdalizi dhidi ya janga Corona. imminente

Ukanda wa Asia-Pasifiki unakabiliwa na changa moto nyingi kukabiliana kabisa na kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19, Shirika la Afya duniani, WHO limeonya.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo ugonjwa huo umeendelea kushika katika katika nchi za ukanda huo na maambukizi ya ndani yameendelea kuripotiwa kwa wingi, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema Jumaane wiki hii.

Licha ya hatua zote zilizochukuliwa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, hatari ya maambukizi katika ukanda huo haitodhibitiwa hadi janga hilo litakapomalizika kabisa, amesema Takeshi Kasai, mkurugenzi wa Shirika la Afya Dunia, WHO, katika ukanda wa Pasifiki ya Magharibi.

"Hii itakuwa vita ndefu na hatuwezi kupunguza ulinzi wetu," Takeshi Kasai amesema katika mkutano na waandishi wa habari, kwa mujibu wa shirika la Habari al Reuters.

"Kila nchi inapaswa iendelee kujiandaa kwa maambukizi ya ndani," Takeshi Kasai ameongeza.

Kasai ameonya kwamba kupungua kwa visa vipya vya maambukizi hakutapelekea kukukosa kuwa makini.