DUNIA-IMF-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapanda, IMF yaonya kuhusu uchumi

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, Kristalina Georgieva, ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020 huku 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani.
Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, Kristalina Georgieva, ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020 huku 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani. REUTERS/Yuri Gripas

Wakati idadi ya vifo inakaribia kufikia 100,000 kutokana na ugonjwa wa Covid-19, Jumuiya ya kimataifa inatafuta jawabu la pamoja la kiuchumi na kidiplomasia kuhusu janga hilo, ambalo linatishia ulimwengu kwa kiasi kikubwa.

Matangazo ya kibiashara

Nchi nyingi kwa sasa ziko hatarini kuathirika kiuchumi kiutokana na ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Corona.

Zaidi ya watu 94,000 wamefariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19, ambao kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgiaieva, utasababisha "athari mbaya zaidi za kiuchumi kama ile iliyoteka mwaka 1929.

Kristalina Georgieva ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020 huku 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani.

Takwimu zingine za kutia moyo barani Ulaya na Marekani zinatoa matumaini ya kupungua idadi ya vifo katika siku za usoni ikilinganishwa na ile iliyotangazwa awali. Kwa mara ya kwanza, idadi ya wagonjwa katika wodi ya wagonjwa mahututi wa Corona imepungua nchini Ufaransa, na wagonjwa wa Corona wanaendelea vizuri nchini Marekani.

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa amezitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kusaidia makampuni ya kibiashara ili kuepusha athari kwa uchumi na kufanya iwe vigumu kuufufua baada ya janga hili kumalizika.

Wiki ijayo kutakuepo na mikutano kati ya IMF na Benki ya Dunia, ambayo itaandaliwa kwa njia ya video kutokana na vizuizi vilivyowekwa kutokana na COVID-19.